Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 37 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi Aliyetakasika na Kutukuka, kisha atamuwekea pazia lake, hapo atamuonyesha wazi madhambi yake ili akiri, kisha atasema: Je wayajua? Atasema: Ndiyo Mola wangu ninayajua, atasema: Basi hakika mimi nilikusitiri madhambi haya ulipokuwa duniani, na mimi ninakusamehe madhambi hayo leo hii, hapo atapewa faili la mema yake, na ama makafiri na wanafiki, wataitwa hadharani mbele ya kadamnasi, (kisha patasemwa) hawa ndio waliompinga Mwenyezi Mungu"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera Ama kafiri hulishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, mpaka akifika Akhera anakuwa hana jema lolote ambalo atalipwa nalo."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
“Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni, hawatokwenda haja ndogo wala kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao vitakuwa vya dhahabu, jasho lao litakuwa ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vikinukia udi wenye harufu nzuri mno, udi wa marashi, na wake zao watakuwa ni katika Mahurulaini, na wote watakuwa katika umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam, urefu kwenda juu ni dhiraa sitini (Dhiraa moja ni inchi 18)".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake