Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 6 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao, hivyo, nikiwakatazeni jambo basi liepukeni, na nikiwaamrisha jambo lifanyeni kadiri muwezavyo"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
“Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakuna yeyote katika Manabii isipokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu, na hakika niliyopewa mimi ni wahyi (ufunuo) wa Mwenyezi Mungu alionifunulia, basi nataraji kuwa na wafuasi wengi kuliko wao siku ya Kiyama".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake