Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 8 kati ya 839

Ondoa vichujio
Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi.
Sahihi Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni kana kwamba katoa sadaka ya ng'ombe, na atakayetoka katika saa ya tatu ni kana kwamba katoa sadaka ya kondoo, na atakayetoka katika saa ya nne ni kana kwamba katoa sadaka ya kuku, na atakaye kwenda katika saa ya tano ni kama katoa yai, akitoka imamu Malaika wanahudhuria kusikiliza ukumbusho".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilimuandalia kuoga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamfunika nguo, na akamimina maji juu ya mikono yake na akaiosha, kisha akamimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, kwa hiyo, akaosha sehemu zake za siri na kuzisafisha, akapiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha, kisha akasukutua kinywa chake na akapandisha maji puani, na akaosha uso na mikono, kisha akamwagia maji kichwani kwake na akaeneza mwili mzima, kisha akasogea pembeni na akaosha miguu yake, nikampa nguo, lakini hakuichukua, akaondoka huku akifuta mikono yake.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga, kisha anaachanisha nywele zake kwa mkono wake, mpaka pale anapohisi kuwa ngozi yake yote imeenea maji, anajimwagia maji kwa michoto mitatu, kisha anaosha mwili wake wote uliobakia, na Aisha akasema: Nilikuwa nikioga mimi na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja, tukichota sote katika chombo hicho.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy