Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 2 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Alituma kikosi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuweka kiongozi bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina), na akawaamrisha wamtii, akachukia, akasema: Hivi hakukuamrisheni Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Ndivyo, akasema: Nikusanyieni kuni, wakakusanya, akasema: Niwashieni moto, wakauwasha, akasema: Ingieni humo, wakataka kuuingia, baadhi yao wakaanza kuwashika wenzao, huku wakisema: Tumeukimbia moto tukaelekea kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, waliendelea katika hali hiyo mpaka moto ukazima, zikatulia hasira zake, habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Laiti wangeingia wasingelitoka humo mpaka siku ya Kiyama; Utiifu unakuwa katika jambo jema".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake