Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 85 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (52)
"Kila wema ni sadaka"
Sahihi Imepokelewa na Bukhari kutokana na hadithi ya Jaabir, na amepokea Muslim kutokana na hadithi ya Hudhaifa
التصنيف الشرعيفضائل الأعمال الصالحة، صدقة التطوعموضوعات الحديثحسن الخلق، الإحسان إلى الخلق، صدقة التطوعمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق
Ally bin Abii Twalib alisema kuniambia: Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعياللباس والزينة، أحكام ومسائل متعلقة بالأمر بالمعروف والنهي عن المنكر، حمل الميت ودفنه، توحيد الألوهيةموضوعات الحديثأحكام المقابر، صنع التماثيل، التصوير، اتخاذ القبور مساجد
"Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيآداب الدعاء، أسباب إجابة الدعاء وموانعه، صفة الصلاة، أذكار الصلاة، صلاة التطوعموضوعات الحديثالدعاء، صفة الصلاة
Alikuwa bin Zubairi akisema mwisho wa kila swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, Laa haula walaa quwwata illaa billaah, Laa ilaaha illa llaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun-ni'matu walahul-fadhlu walahuth-thanaaul hasan, Laa ilaaha illa llaahu Mukhliswiina lahud-diina walau karihal kaafiruun" Na akasema: "Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيأذكار الصلاةموضوعات الحديثالذِّكْر، الأذكار الشرعية
"Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu. kisha akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, Akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, kisha akasema: Hayya ala Swalaah, akasema: Laa Haula wala Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Hayya ala lfalaah, akasema: Laa Haula walaa Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Laa ilaha ila llahu, akasema: Laa ilaha ila llahu, kutoka ndani ya moyo wake, basi ataingia peponi".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفضل الذكر، الأذان والإقامةموضوعات الحديثالذِّكْر، أحكام الأذان والإقامة
"Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفضائل أعمال الجوارح، الوضوء
Hakika mama Habiba bint Jahshi aliyekuwa chini ya Abdulrahman bin Auf alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu damu, akasema kumwambia: "Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga". Akawa akioga kila wakati wa swala.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالحيض والنفاس والاستحاضةموضوعات الحديثأحكام الغسل، أحكام الحيض والنفاس، أحكام الاستحاضة
Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيسنن الفطرة والسواك