Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 28 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
"Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."
Sahihi Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike, na katika kila arobaini mwenye miaka miwili, na kutoka kwa kila anayeishi humo asiye muislamu Dinari au kitu chenye thamani sawa na Dinari kama Maafiri, nazo ni nguo hutengenezwa Yemen.
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
"Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Alitufundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hotuba ya dharura (Haja)" Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, tunamtaka msaada na tunamuomba msamaha, na tunajilinda kwake kutokana na shari ya nafsi zetu, anaye muongoza Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na anayempoteza hakuna wa kumuongoa, na ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na nina shuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, "Enyi watu mcheni Mola wenu aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akaiumbia mke wake, na akatoa kutoka kwa wawili hao wanaume wengi na wanawake wengi, na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnaombana kwa jina lake nyinyi na familia zenu, hakika Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mchunga" [An-Nisaai:1] "Enyi mlio amini mcheni Mwenyezi Mungu ukweli wa kumcha, na wala msife ila mfe nanyi ni waislamu (wa kweli)" [Al-Imran: 102], "Enyi mlio amini mcheni Mwenyezi Mungu na mseme maneno ya sawa (70) Atakutengenezeeni mambo yenu na atakusameheni madhambi yenu, na atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume atakuwa amefaulu kufaulu kukubwa" [Al-Ahzaab: 70-71].
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
"Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Nilikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika kundi la wanawake ili wampe ahadi ya utiifu (Baiaa) wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunakupa ahadi juu ya kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na tusizini, na tusilete uzushi tutakaouzua mbele ya mikono yetu na miguu, na wala tusikuasi katika jema lolote, akasema: "Katika yale mnayoyaweza, na mkayahimili" Anasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanahuruma zaidi kwetu, njoo tukupe ahadi ya utiifu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi siwapi mkono wanawake, bali hakika kauli yangu kwa wanawake mia moja ni sawa na kauli yangu kwa mwanamke mmoja, au ni mfano wa kauli yangu kwa mwanamke mmoja".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah