Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 38 kati ya 839

Ondoa vichujio
Alitusalisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya asubuhi, akasema: "Hivi fulani yupo", Wakasema: Hapana, akasema: "Na je fulani yupo?", Wakasema: Hapana: Akasema: "Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti, na hakika safu ya kwanza iko katika mithili ya safu ya Malaika, na laiti mngejua ni zipi fadhila zake basi mngezijia haraka mno, na hakika swala ya mtu na mwenzie ni safi zaidi kuliko swala yake peke yake, na swala yake akiwa na watu wawili ni nzuri zaidi kuliko swala yake na mtu mmoja, na wingi unavyozidi ndio unaopendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na Ahmad
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud kwa matamshi haya, na amepokea Bukhari bila ya kuzidisha (baada ya kutwaharika)
"Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi mungu kuliko siku hizi" Yaani: Siku kumi (za mwanzo wa Dhul-Hija), Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake na hakurudi na chochote katika hivyo".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Abu Daud na matamshi ya hadithi ni yake
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud