Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 10 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".
Sahihi Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim, na matamshi haya ni ya Muslim, na akaipokea Bukhari kwa ufupi.
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako" Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika kukutii".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuja bedui kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: Nifundishe maneno nitakayoyasema. Akasema "Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima" Akasema: Haya ni kwa ajili ya Mola wangu, yako wapi ya kwangu? Akasema: "Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi na unihurumie na uniongoze na uniruzuku".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim