Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 53 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
"Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama" Yaani: Upepo yake.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba: Alituamrisha kumtembelea mgonjwa, na kusindikiza jeneza, na kumuombea mwenye kupiga chafya, na kukiepusha kiapo au kumuepusha (na tuhuma) aliyeapa, na kumnusuru aliyedhulumiwa, na kuitika wito wa mwenye kualika (au kuita), na kutoa salamu, na akatukataza kuvaa pete za dhahabu, na kunywa katika vyombo vya madini ya fedha, na kukalia matandiko ya hariri, na kuvaa kassi (nguo iliyotengenezwa kwa katani na hariri) na kuvaa hariri nyepesi na hariri nzito na dibaji.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Alikaa itikafu Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akawasikia wakidhihirisha kisomo, akafunua pazia, akasema: "Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi, na wasinyanyue sauti baadhi yenu kwa wenzao katika kisomo", au alisema: "Katika swala".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud
"Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake