Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 6 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud
Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud
"Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahlii abwaaba rahmatika, (Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: Allaahumma'swimnii minash-shaitwaanir-rajiim", (Ewe Mwenyezi Mungu nikinge dhidi ya Shetani aliyelaaniwa. Na katika riwaya ya Al-Haakim: "Na akitoka amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu nilinde dhidi ya Shetani aliyelaaniwa".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Ibn Majah na Alhakim
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfir lii, warhamnii, wa aafiniii, wahdinii, warzuqniii".
Ni Nzuri kwa Ushahidi wake mbalimbali Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad