عربي - Arabic English Qafár af - Afar Afrikaans - Afrikanns Akan Shqip - Albanian አማርኛ - Amharic Հայերեն - Armenian অসমীয়া - Assamese Azərbaycanca - Azerbaijani Bamanankan - Bambara Bassa Bemba বাংলা - Bengali Bosanski - Bosnian Български - Bulgarian မြန်မာဘာသာ - Burmese Bisaya - Cebuano Cham Нохчий - Chechen chiCheŵa - Chewa 中文 - Chinese Адыгэбзэ - Circassian Hrvatski - Croatian Česky - Czech Dagbani Dansk - Danish فارسی دری - Dari Dendi ދިވެހި ބަސް - Dhivehi Nederlands - Dutch إستوني - Estonian Suomi - Finnish Français - French Fulfulde - Fula ქართული - Georgian Deutsch - German Ελληνικά - Greek ગુજરાતી - Gujrati Kreyòl ayisyen - Haitian Creole Hausa हिन्दी - Hindi Magyar - Hungarian Igbo Indonesia - Indonesian Italiano - Italian 日本語 - Japanese Jóola - Jola ಕನ್ನಡ - Kannada Қазақша - Kazakh ភាសាខ្មែរ - Khmer Kikuyu Ikinyarwanda - Kinyarwanda Ikirundi - Kirundi 한국어 - Korean كوردی سۆرانی - kurdish كوردي kurmancî - Kurmanji Kyrgyz ລາວ - Lao latviešu - Latvian Lingala lietuvių - Lithuanian Luganda Македонски - Macedonian Maguindanaon Malagasy - Malagasy Bahasa Melayu - Malay മലയാളം - Malayalam Mandinka मराठी - Marathi Mõõré - Moore नेपाली - Nepali أنكو - NKo Norwegian ଓଡ଼ିଆ - Odia oromoo - Oromo پښتو - Pashto فارسی - Persian Polski - Polish Portuguese ਪੰਜਾਬੀ - Punjabi Română - Romanian Русский - Russian Српски - Serbian Shona සිංහල - Sinhala Slovenščina - Slovenian Soomaaliga - Somali Soninke Sesotho - Sotho Español - Spanish Kiswahili - Swahili Svenska - Swedish Tagalog Тоҷикӣ - Tajik தமிழ் - Tamil తెలుగు - Telugu ไทย - Thai ትግረኛ - Tigrinya Türkçe - Turkish Ukrainian اردو - Urdu ئۇيغۇرچە - Uyghur Ўзбек - Uzbek Việt Nam - Vietnamese Wolof Yao Yorùbá - Yoruba Zarma زولو - Zulu
839 Hadithi
Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii
Makundi
Daraja la hadithi
Imesimuliwa katika
Onyesha vyanzo vilivyobaki
Msimulizi
Katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji:25] Akasema: "Lau kama mtu atadhamiria ubaya akiwa katika mji wa eden (Yemen) mbali huko, basi Mwenyezi Mungu angemuonjesha adhabu chungu".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad na Al Hakim
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka aliteremsha "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri" [Maaida: 44] na "basi hao ndio madhalimu" [Maida: 45] na "basi hao ndio waovu" [Maida: 47], akasema: Amesema bin Abbasi: Aliziteremsha Mwenyezi Mungu kwa makundi mawili katika Mayahudi, na moja lilikuwa limelitenza nguvu jingine katika zama za ujinga, mpaka wakaridhiana na wakapatana kuwa kila dhalili aliyeuliwa na mtu mtukufu fidia yake ni Waski hamsini, sawa na (kg 6100), na kila maiti aliyeuliwa na mtu dhalili katika watukufu basi fidia yake ni Waski mia moja (100) sawa na (kg12,200), na walikuwa wakiishi katika maisha hayo mpaka alipokuja Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mji wa Madina, na makundi yote mawili yakajishusha kwa kufika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati huo hajajulikana kwa watu, na hakuwa amewalazimisha na kuwatenza nguvu katika hilo, na huo ulikuwa ni wakati wa ule mkataba wa maridhiano (Hudaibia), basi mtu dhalili akamuuwa mtukufu mmoja, basi yule mtukufu akatuma ujumbe kwa ndugu wa yule dhalili kuwa tunataka mtuletee Waski mia moja (kg12,200) yule dhalili akasema: Je ni kweli ndivyo ilivyokuwa katika mitaa yao kwamba dini yao ni moja, na nasaba yao ni moja, na mji wao ni mmoja, kwamba fidia ya baadhi yao ni nusu ya wenzao? Bila shaka hakika sisi tumekupeni kiasi hicho kwa kutudhulumu, na kwakuwa tunawaogopa, ama kwakuwa Muhammadi amekuja hatutokupeni, basi vita ikakaribia kuwaka baina yao, kisha wakaridhiana kuwa wamfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muamuzi wao, kisha yule mtukufu akaanza kueleza na akasema: Wallahi Muhammadi hatokupeni toka kwao zaidi ya kile atakachowapa toka kwenu, na hakika wamesema kweli, hawakutupa isipokuwa kwa dhuluma na kwa kutuogopa sisi, na kuwatenza nguvu, basi tumeni kwa Muhammadi mtu atakayekuleteeni maoni yake: Ikiwa atakupeni mnachotaka basi mfanyeni kuwa hakimu wenu, na asipokupeni basi muepukeni na msimfanye kuwa hakimu, basi wakatuma kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu miongoni mwa wanafiki ili wawaletee habari na maoni ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Mwenyezi Mungu alimpa habari Mtume wake ya jambo lao lote na kile walichokitaka, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale ambao wanakimbilia kuukanusha unabii wako miongoni mwa wanafiki ambao wameonyesha Uislamu..." [Maida: 41] Mpaka katika kauli yake: "Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio mafasiki (waovu)" [Maida: 47] Kisha akasema kuhusu aya hizo, Wallah zimeteremka, na bila shaka wao ndio Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakusudia.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Ahmad