Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".
«إِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ».
Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kupiga mwayo pale alipofungua kinywa chake kwa sababu ya uvivu au kujaa na mfano wake; kuwa aweke mkono wake juu ya kinywa chake ili akifunge kwa mkono; na hii ni kwa sababu Shetani huingia ndani yake anapokiacha wazi, kuweka mkono kunakuwa ni kizuizi cha kumzuia kuingia.
Atakapotaka mtu kupiga miayo anatakiwa auzuie kwa kadiri awezavyo, kwa kuuzuia mdomo wake, na aubakishe ukiwa umefungwa wala usifunguke, asipoweza kuubakisha mdomo wake ukiwa umefungwa basi aweke mkono wake juu ya mdomo wake, afunike kinywa chake kwa mkono wake.
Kushikamana na adabu za kiislamu katika hali zote; kwa sababu ndio anwani ya ukamilifu na tabia njema.
Kuchukua tahadhari ya kila mapitio ya Shetani kwa mwanadamu.
Swahiih Muslim (4/ 2293) (2995).
Zaidi (8)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (2/ 151).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (4/ 436).
تطريز رياض الصالحين.
لفيصل آل مبارك (ص529).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
مجموعة من الباحثين (1/ 679).
Imenukuliwa katika vitabu
3 VitabuZaidi (3)
- تحفة الأخيار تحفة الأخيار (ببيان جملة نافعة مما ورد في الكتاب والسنة من الأدعية والأذكار)«إِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ، فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ» [96]
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 5«إذَا تَثَاءَبَ أحَدُكُمْ فلْيُمْسكْ بيَدِه عَلَىٰ فيهِ، فإنَّ الشَّيْطانَ يَدْخُلُ».
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (3)، والسيرة النبوية (3)التربية الإٍسلامية -3- «إِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ، فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ»