Skip to content

Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto

Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema:

"Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".

«إِذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ فَلْيَأْكُلْ بِيَمِينِهِ، وَإِذَا شَرِبَ فَلْيَشْرَبْ بِيَمِينِهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِشِمَالِهِ، وَيَشْرَبُ بِشِمَالِهِ».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Anamuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu ale na anywe kwa mkono wake wa kulia, na anakataza kula na kunywa kwa mkono wa kushoto; na hii ni kwa sababu Shetani anakula na anakunywa kwa kushoto.

Katika Faida za Hadithi

Katazo la kujifananisha na Shetani kwa kula au kunywa kwa kushoto.

Rejea

Swahiih Muslim (3/ 1598) (2020).

Zaidi (8)

توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.

للبسام (5/ 445).

فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام.

لابن عثيمين (6/ 270).

سبل السلام شرح بلوغ المرام.

للصنعاني (2/ 625).

عون المعبود شرح سنن أبي داود (10/ 179).

فتاوى اللجنة الدائمة - المجموعة الأولى- (26/ 387).