Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 86 kati ya 839

Ondoa vichujio

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (53)
"Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy
"Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi".
Sahihi Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
"Hakika umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu bila kumshirikisha na chochote, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhiji. kisha akasema Mtume: Je, nikujulishe milango ya kheri? Funga ni kinga, na sadaka inaondosha madhambi kama maji yanavyo uzima moto, na swala ya mtu katikati ya usiku, kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mbavu zao zinaachana na vitanda..." mpaka alipofikia mwisho wa aya "wanayoyatenda". Kisha akasema Mtume: Je nikueleze kichwa cha mambo yote na nguzo yake na kilele chake? Nikajibu ndio ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: kichwa cha mambo yote ni Uislamu, na nguzo yake ni Swala, na kilele chake ni Jihadi. Kisha akasema: Je nikujulishe kinachoyahifadhi na kuyatunza matendo hayo? Nikasema ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akaushika ulimi wake kisha akasema: Zuia ulimi wako, nikamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je tutahesabiwa kwa kila tunacho kizungumza? Akasema: Akukose mama yako, hakuna kitakacho waingiza watu wengi motoni kama maneno wanayoyazungumza."!
Sahihi Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
"Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana".
Sahihi kwa mkusanyiko wa njia zake Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Je, nisikuelezeni mbora wenu na muovu wenu?" Anasema: Wakanyamaza, akalisema hilo mara tatu, mtu mmoja akasema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tueleze mbora wetu na muovu wetu, akasema: "Mbora wenu ni yule inayetarajiwa heri yake, na kuaminiwa kutokuwepo kwa shari yake, na muovu wenu ni yule isiyetarajiwa heri yake, na kutoaminiwa shari yake".
Sahihi Imepokelewa Imamu Tirmidhiy