Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 54 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Laiti nyinyi mgetegemea kwa Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, wanarudi jioni wakiwa wameshiba".
Sahihi Imepokelewa na Imam Ahmad, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ibn Hibban katika Sahih yake na Haakim
"Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ibn Hibban
"Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
“Je, nisiwaambieni matendo bora zaidi kwenu, na masafi zaidi mbele ya Mfalme wenu, na yatakayo kunyanyueni juu zaidi katika daraja zenu, na bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na pesa, na bora kwenu kuliko hata kukutana na adui yenu na mkapiga shingo zao na wakapiga shingo zenu?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: “Ni kumtaja Mwenyezi Mungu".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
"Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad