Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 7 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (57)
"Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"
Sahihi Imepokelewa na Ibn Majah na Ahmad
"Mswaki ni usafi wa kinywa, humridhisha Mola".
Sahihi Imepokelewa na Nasai na Ahmad
"Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Nilisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia kadhaa wa kadhaa, (Anasema mmoja wa wapokezi wa hadithi hii: Alikuwa akikusudia ufupi) Akasema: "Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo" Akasema Aisha: Na nikamsimulia kuhusu mtu fulani, akasema: "Sipendi kuona kuwa kuna mtu nimemsimulia na kwamba mimi nina kadhaa wa kadhaa".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad