Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 85 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"
Sahihi Imepokelewa na Ibn Majah na Ahmad
"Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana".
Sahihi kwa mkusanyiko wa njia zake Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad