Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 33 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy
التصنيف الشرعيالأخلاق الحميدة، الأخلاق الذميمة، آداب الكلام والصمتموضوعات الحديثحفظ اللسان، حسن الخلقمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق
"Atakayeswali swala ya Asubuhi basi huyo yuko katika dhima ya Mwenyezi Mungu, basi asikukoseni Mwenyezi Mungu kwa chochote katika dhima yake, na atakayetafutwa na Mwenyezi Mungu katika dhima yake kwa chochote humdiriki (humuadhibu), kisha humburuza kwa uso wake motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيوجوب الصلاة وفضلها وحكم تاركهاموضوعات الحديثالظلم، معاداة أولياء الله وأذيتهم، مكانة الصلاة وفضلها
"Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
التصنيف الشرعيالهجرة وأحكامها، الأخلاق الحميدة، آداب الكلام والصمت، ذم المعاصي، الإسلامموضوعات الحديثحفظ اللسان، حسن الخلق، التقوىمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق
"Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
التصنيف الشرعيأحكام الإمامة، حقوق الرعية على الإمامموضوعات الحديثالغش، أحكام الإمامةمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق، عدل الإسلام
"Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
التصنيف الشرعيذم المعاصي، ذم حب الدنيا، أحكام الإمامةموضوعات الحديثأكل أموال الناس بالباطل، الظلم، أحكام الإمامة
"Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye".
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali Imepokelewa na Addar- Alqutni
التصنيف الشرعيالقواعد الفقهية والأصوليةموضوعات الحديثالظلم، الإحسان إلى الخلقمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق، عدل الإسلام
"Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيأحكام النساء، ذم حب الدنيا، ذَمُّ الهوى والشَّهواتموضوعات الحديثالزهد وقِصَر الأمل، التقوى
"Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
التصنيف الشرعيالأخلاق الحميدة، العشرة بين الزوجين، الإيمانموضوعات الحديثحسن الخلق، حق الزوجةمحاور التعريف بالإسلاممحاسن الأخلاق