Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 6 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad
التصنيف الشرعيزيارة القبور، أحكام المساجد، الشركموضوعات الحديثأحكام المساجد، اتخاذ القبور مساجد
Yakuwa Mtume rehema na amani zimfikie alipotoka kwenda katika vita vya Hunaini alipita katika mti wa washirikina ukiitwa: Dhata anwatwi (Mahala pa kutundika silaha) wakitundika silaha zao hapo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tuwekee nasi mahala pa kutundikia kama ambavyo wao wana mahala pa kutundikia, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Maneno haya ni kama yale waliyosema watu wa Mussa: "Tufanyie nasi mungu kama walivyo wao na mungu" [Al-A'raaf: 138] Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
التصنيف الشرعيأحكام التشبه، توحيد الألوهية، تفسير الآيات، الشركموضوعات الحديثالتشبه بالكفار، الشرك بالله وأقسامهمحاور التعريف بالإسلامبطلان الشرك وصوره
"Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".
Sahihi kwa mkusanyiko wa njia zake Imepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na Ahmad
التصنيف الشرعيآداب الكلام والصمت، توحيد الألوهية، الشركموضوعات الحديثحفظ اللسان، أهمية التوحيد، الشرك بالله وأقسامه
"Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
التصنيف الشرعيفضائل أعمال القلوب، أعمال القلوب، الشركموضوعات الحديثأهمية التوحيد، الشرك بالله وأقسامه، التوكل
"Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
التصنيف الشرعيالشركموضوعات الحديثأهمية التوحيد، السحر، الكهانة والعرافة والتنجيم وإتيان من يتلبس بهذه المنكراتمحاور التعريف بالإسلامبطلان الشرك وصوره
"Hakika katika watu waovu zaidi ni wale watakaokutwa na Kiyama wakiwa hai, na mwenye kuyafanya makaburi kuwa mahala pa kusalia".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Ahmad
التصنيف الشرعيأحكام المساجد، أشراط الساعة، الشركموضوعات الحديثأشراط الساعة، اتخاذ القبور مساجد