Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 20 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu, basi ataambiwa: Hivi unajua waliyoyafanya baada yako? Namuapia Mwenyezi Mungu, hawakuacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu, kwani mimi nilisikia mkanyago wa viavu vyako mbele yangu huko Peponi" Akasema: Sijawahi kufanya amali yoyote yenye matarajio kwangu isipokuwa sijawahi kutia udhu wowote, katika nyakati za usiku au mchana, isipokuwa ninaswali kwa udhu huo kiasi nilichoandikiwa niswali katika rakaa.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Peponi kuna daraja mia moja baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa mbingu na ardhi, na Firdausi iko daraja ya juu zaidi kuliko zote, na ndani yake ndiko inako chimbuka mito yote minne ya pepo, na juu yake ndiko inakokuwa Arshi, Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi".
Sahihi Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
"La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera Ama kafiri hulishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, mpaka akifika Akhera anakuwa hana jema lolote ambalo atalipwa nalo."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake."
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni, hawatokwenda haja ndogo wala kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao vitakuwa vya dhahabu, jasho lao litakuwa ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vikinukia udi wenye harufu nzuri mno, udi wa marashi, na wake zao watakuwa ni katika Mahurulaini, na wote watakuwa katika umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam, urefu kwenda juu ni dhiraa sitini (Dhiraa moja ni inchi 18)".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake