Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 14 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Jua litasogezwa karibu na viumbe Siku ya Kiyama mpaka liwe karibu nao umbali wa maili moja.", Sulaim bin 'Amir akasema: "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sijui (kiwango) alimaanisha nini kwa "maili"? Je, ni umbali katika ardhi au ni kile kijiti kinachotumiwa kupaka wanja wa manga kwenye jicho." (Mtume) Akasema: "Kisha, watu watakuwa ndani ya jasho yao kulingana na matendo yao. Miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye vifundo viwili vya miguu yake. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye magoti yake mawili. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye nyonga zake mbili. Na miongoni mwao, kuna ambaye jasho (lake) litammeza kabisa."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika, mwenye kiwango cha chini zaidi kati yenu katika Pepo ni kwamba ataambiwa: "Tamani!" Basi atatamani na atamani, na ataambiwa: "Je umeshatamani?" Atasema: "Nidyo." Ataambiwa: "Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akautazama mwezi usiku (yaani: Usiku wa tarehe 15) akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kufanya hima msizidiwe mkashindwa kusali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" Kisha akasoma: "Na umtukuze Mola wako kwa himdi zake njema kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni, basi litachemshwa katika moto wa Jahanam, kisha zitapigwa pasi mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila linapopoa linarejeshewa umoto, katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, (atadumu katika adhabu hiyo) mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake, ima inakwenda peponi, na ima anakwenda motoni"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja, kila mmoja anamtazama mwenzake? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Aisha, jambo litakuwa kubwa mno, kuliko hata mtu kushughulika kumtazama mwenzake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Je mnajua ni nani aliyefilisika?" Wakasema: Aliyefilisika kwetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na Dirham (pesa) wala mali yoyote. Akasema: "Hakika aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya Kiyama akiwa na (ibada za) swaumu na swala na zaka, na akaja akiwa kamtukana huyu, na kamzulia machafu huyu, na kala mali ya huyu, na amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, hivyo atapunguziwa huyu kutoka katika mema yake, na huyu katika mema yake, yakimalizika mema yake kabla hajamaliza kulipa anayodaiwa yatachukuliwa kutoka katika makosa yao yatatupwa kwake kisha atatupwa katika moto".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim