Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 7 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Hakika mimi sikutumwa kuwa mtoa laana, bali nilitumwa kuwa huruma".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ya kwamba kuna kundi miongoni mwa wanafunzi wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliwauliza wake za Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu amali zake za siri? (walipojibiwa) wakasema baadhi yao: Mimi sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Na mimi sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala juu ya godoro. Hilo likamfikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifia, na akasema: "Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Hakuwahi kula Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake milo miwili kwa siku isipokuwa mlo mmoja utakuwa ni tende.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende, na katika riwaya ya Muslim: ulikuwa mto wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliokuwa akiegamia umetokana na ngozi ndani umejazwa majani.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake