Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 4 kati ya 839

Ondoa vichujio
Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake."
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu, zikamateni na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharini na mambo ya kuzushwa. Kwani kila jambo jipya (katika dini) ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu."
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy
Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka kwa ajili ya haja yake, tukaona ndege akiwa na makinda mawili, tukawachukua makinda wake, akaja yule ndege akaanza kupepesa mbawa zake, basi akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha ndege huyu kwa mwanaye? Mrejesheeni mwanaye", na akaona kijiji cha wadudu chungu tulichokichoma kwa moto, akasema: "Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud