Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 72 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja humuita Jibril na husema: Hakika mimi ninampenda fulani basi mpende, anasema: Jibril humpenda, kisha anaita huko mbinguni na kusema: Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani basi mpendeni, wanampenda wakazi wa mbinguni, anasema kisha anapewa kukubalika katika Ardhi, na anapomchukia mja humuita Jibril na kusema: Hakika mimi ninamchukia fulani basi mchukie, anasema; Basi Jibril humchukia, kisha ananadi kwa wakazi wa mbinguni; hakika Mwenyezi Mungu anamchukia fulani basi mchukieni, anasema: basi wanamchukia, kisha anawekewa kuchukiwa katika Ardhi".
Sahihi Swahiih Muslim
"Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo, na ama kunipinga kwake ni kauli yake: Mwenyezi Mungu hatonirudisha kuwa hai, kama alivyonianzisha, na si kuanza kuumba ni kwepesi zaidi kwangu kuliko kurudisha, na kunitukana kwake ni kauli yake: kuwa Mwenyezi Mungu kajifanyia mwana, na mimi ndiye mmoja mwenye kukusudiwa, sikuzaa wala sikuzaliwa, na wala hakuna anayefanana nami hata mmoja".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuja kwake kundi, akawaunga mkono watu tisa na akamuacha mmoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewaunga mkono watu tisa na ukamuacha huyu? akasema: "Huyo yuko na hirizi", akaingiza mkono wake akaikata, akamuunga mkono, akasema: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina"
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Ahmad