Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 7 kati ya 839

Ondoa vichujio
Yakuwa Mtume rehema na amani zimfikie alipotoka kwenda katika vita vya Hunaini alipita katika mti wa washirikina ukiitwa: Dhata anwatwi (Mahala pa kutundika silaha) wakitundika silaha zao hapo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tuwekee nasi mahala pa kutundikia kama ambavyo wao wana mahala pa kutundikia, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Maneno haya ni kama yale waliyosema watu wa Mussa: "Tufanyie nasi mungu kama walivyo wao na mungu" [Al-A'raaf: 138] Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".
Sahihi kwa mkusanyiko wa njia zake Imepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na Ahmad
"Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad
"Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni."
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Upokezi wake ni mzuri رواه ابن ماجه والنسائي في الكبرى وأحمد
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".
Sahihi Imepokelewa na Muslim na Ahmad
Yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuja kwake kundi, akawaunga mkono watu tisa na akamuacha mmoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewaunga mkono watu tisa na ukamuacha huyu? akasema: "Huyo yuko na hirizi", akaingiza mkono wake akaikata, akamuunga mkono, akasema: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina"
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Ahmad