Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 3 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (54)
"Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi, kukawa na kundi moja zuri lililokubali maji likaotesha malisho na majani mengi, na ilikuwa ni ardhi ni kame iliyomeza maji Mwenyezi Mungu akanufaisha watu kupitia ardhi hiyo wakanywa na wakanywesha na wakalima, na mvua hiyo ikashuka katika sehemu nyingine ya ardhi laini haitulizi maji na wala haioteshi mimea; Huu ndio mfano wa mtu aliyejifunza akaelimika katika dini ya Mwenyezi Mungu na yakamnufaisha aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu akajua na akafundisha, na mfano mwingine ni wa mtu ambaye hakuyatilia maanani na wala hakukubali uongofu wa Mwenyezi Mungu ambao nimetumwa nao".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake