Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 3 kati ya 839

Ondoa vichujio
Filter
Pick a property to filter by
الفئة المستهدفة1
حجم المحتوى3
التخريج المتعدد2
حجم المحتوى: متوسط

Daraja la hadithi

Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina muongozaji wa kunileta msikitini, akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amruhusu asali nyumbani kwake, akamruhusu, alipoondoka akamuita, akasema: "Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالأذان والإقامة، فضل صلاة الجماعة وأحكامها، صلاة أهل الأعذارموضوعات الحديثأحكام الأذان والإقامة، صلاة الجماعة، صلاة أهل الأعذار
"Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفضائل الأعمال الصالحة، فضل الوضوء، سنن وآداب الوضوء، وجوب الصلاة وفضلها وحكم تاركها، فضل صلاة الجماعة وأحكامها، أحكام المساجدموضوعات الحديثأحكام المساجد غير الحرمين، أحكام الوضوء، مكانة الصلاة وفضلها، صلاة الجماعة
"Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
التصنيف الشرعيوجوب الصلاة وفضلها وحكم تاركها، فضل صلاة الجماعة وأحكامها، النفاقموضوعات الحديثصلاة الجماعة