Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 5 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala, pindi anapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linafunguka fundo moja, akitawadha, linafunguka fundo jingine, na akiswali, yanafunguka mafundo yake yote, anaamka akiwa na uchangamfu na moyo mkunjufu, na vinginevyo basi anaamka akiwa na nafsi chafu tena mvivu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala, nikasema: Nyinyi mlikuwa mnafanya vipi? Akasema: Ulikuwa ukimtosha mmoja wetu udhu mmoja madam hajatengukwa.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi, na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye huiuza nafasi yake yuko anayeikomboa kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim