Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 19 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende, na katika riwaya ya Muslim: ulikuwa mto wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliokuwa akiegamia umetokana na ngozi ndani umejazwa majani.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake