Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 5 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake."
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Kusimzuie mmoja wenu kuwaogopa watu akaache kusema haki atakapoiona au kuijua".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake, na wala hatokunywa katika Hodhi langu, na ambaye hatowaamini kwa uongo wao na akawa hakuwasaidia katika dhulma yao, basi huyo yuko miongoni mwangu, na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad