Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 24 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni ni yule atakayekuwa na viatu viwili na soli mbili vitokanavyo na moto, utakuwa ukitokota kwa hivyo ubongo wake kama kinavyotokota chungu, hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali kuliko yeye, kumbe yeye ndiye ana adhabu nafuu kuliko wote"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
“Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni, hawatokwenda haja ndogo wala kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao vitakuwa vya dhahabu, jasho lao litakuwa ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vikinukia udi wenye harufu nzuri mno, udi wa marashi, na wake zao watakuwa ni katika Mahurulaini, na wote watakuwa katika umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam, urefu kwenda juu ni dhiraa sitini (Dhiraa moja ni inchi 18)".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy