Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 2 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Imesimuliwa katika

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (34)
Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-katika yale aliyoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu hakika Yeye amesema: "Enyi waja wangu hakika Mimi nimeharamisha dhulma juu ya Nafsi yangu na nikaifanya kuwa ni haramu baina yenu, basi msidhulumiane, enyi waja wangu nyote ni wapotevu isipokuwa yule niliye muongoza, basi niombeni uongofu nami nitakuongozeni, enyi waja wangu nyote ni wenye njaa isipokuwa yule niliye mlisha, basi niombeni chakula nami nitakulisheni, enyi waja wangu nyote mpo uchi isipokuwa yule niliye mvisha, basi niombeni kuvaa nami nitakuvisheni, enyi waja wangu hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitakusameheni, enyi waja wangu hamtafikia kufanya madhara ili mnidhuru wala hamtafanya mambo yenye manufaa ili mninufaishe, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakawa na ucha Mungu wa mtu mmoja hilo lisinge niongezea chochote katika Ufalme wangu chochote, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakafanya uovu wa mtu mmoja hilo lisinge punguza chochote katika Ufalme wangu, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wangejikusanya katika uwanja mmoja wakaniomba nikampa kila mtu alicho kiomba hilo lisinge punguza chochote katika Ufalame wangu isipokuwa ni kama sindano inavyo punguza maji pindi inapo ingizwa baharini, enyi waja wangu si vinginevyo bali hakika matendo yenu yote nina wahifadhieni kisha nitawapa malipo yenu, mwenye kupata kheri amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakayepata kinyume na hayo basi asimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye utajiri: Wanaswali kama tunavyoswali na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka katika mali yao ya akiba. Akasema: Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi yawezekanaje akidhi mmoja wetu matamanio yake kisha awe na malipo? Akasema: Mnasemaje ikiwa atakiweka katika haramu, je atakuwa na mzigo wa dhambi? basi ndivyo hivyo akikiweka katika halali atakuwa na malipo".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim