Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 21 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu. Iliwapelekea kumwaga damu zao, na kuhalalisha yaliyo haramu kwao".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Je mnajua ni nani aliyefilisika?" Wakasema: Aliyefilisika kwetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na Dirham (pesa) wala mali yoyote. Akasema: "Hakika aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya Kiyama akiwa na (ibada za) swaumu na swala na zaka, na akaja akiwa kamtukana huyu, na kamzulia machafu huyu, na kala mali ya huyu, na amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, hivyo atapunguziwa huyu kutoka katika mema yake, na huyu katika mema yake, yakimalizika mema yake kabla hajamaliza kulipa anayodaiwa yatachukuliwa kutoka katika makosa yao yatatupwa kwake kisha atatupwa katika moto".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim