Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 21 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Haingii peponi mfitinishaji".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno, na wala msitiliane shaka (kwa kuhisiana vibaya), na wala msichunguzane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, na wala msichukiane, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Tulikuwa vitani, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mmoja katika Answari, Answari akasema: Maanswari naombeni msaada!, na akasema Mhajiri (mtu wa Makka): Naombeni msaada enyi Muhajirina!, Mwenyezi Mungu akamsikilizisha sauti zile Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Nini hiki?" Wakasema: Mtu mmoja miongoni mwa Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari, akasema Answari: Naombeni msaada enyi Maanswari, na akasema Mhajiri: Naombeni msaada enyi Muhajirina, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Achaneni (na ubaguzi) kwani una nuka" Amesema Jabiri: Na Maanswari walikuwa wengi kipindi alipofika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo, akasema Abdallah bin Ubaiyi: Vipi wamepigana? Na Wallahi tukirejea Madina watukufu watawafurusha madhalili, akasema Omari bin Khattwabi: Naomba uniache mimi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Muache ili watu wasiseme Muhammadi anauwa Maswahaba zake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake