Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 16 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Ya kwamba mtu mmoja alikuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake jina lake anaitwa Abdallah, na alikuwa akitaniwa kwa jina la Punda, na alikuwa akimchekesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa viboko kwa sababu ya ulevi, basi akaletwa siku moja akaamrisha akachapwa, akasema mtu mmoja katika jamaa waliopo: Ewe Mwenyezi Mungu mlaani, ni mara ngapi analetwa!? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy