Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 13 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Alinijia mwanamke mmoja Masikini akiwa amebeba mabinti zake wawili, nikawalisha tende tatu, akawapa kila mmoja wao tende moja, kisha akanyanyua tende moja ili kuitumia , akawalishi mabinti zake kwa kuigawa tende ile vipande viwili, ambayo alihitaji kuila mwenyewe, kikanistaajabisha kitendo chake hicho, nikamueleza Mtume alicho kifanya mwanamke yule, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim