Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 75 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Nilimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanipa, kisha nikamuomba tena akanipa, kisha akasema kuniambia: "Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu, atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa kujikweza hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa sawa na yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini", Hakim anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ninamuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitompunguzia yeyote mali yake baada yako kamwe mpaka ntakapoondoka duniani, akawa Abubakari akimuita Hakim ili ampe chochote, akawa anakataa kupokea chochote kutoka kwake, kisha Omari alimuita ili ampe, akakataa kupokea, akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi ninamletea haki yake ambayo Mwenyezi Mungu kamgawia katika ngawira, anakataa kuichukua. Hakim hakumuomba tena mtu yeyote baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki Mwenyezi Mungu amrehe
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe,kisha muitaji ataita; Enyi watu wa peponi, basi watainua vichwa vyao na kuangalia, basi mwenye kuita atasema: Je mnamjua huyu? Nao watajibu: Ndiyo hayo ni Mauti, na wote kwa hakika wameyaona, kisha mwenye kuita atawaita: Enyi watu wa Motoni, basi watainua shingo zao na kuangalia, basi atawaambia na je mnamjua huyu basi watamjibu ndiyo haya ni Mauti, na wote kwa kakika wameyaona, hivyo basi yatachinjwa kisha atasema: Enyi watu wa Peponi,kaeni humo milele na hakuna kufa, na nyie watu wa motoni kaeni humo milele na hakuna kufa, kisha akasoma: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa Nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" (Surat Maryam:39)
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim