Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 64 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالزهد والورع، ذم حب الدنيا
"Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيأحوال الصالحين
Tulikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku mema elfu moja?" Akamuuliza muulizaji miongoni mwa waliokuwa naye kwenye kikao: "Vipi anaweza kuchuma mmoja wetu mema elfu moja?" Akasema: "Atasema Sub-haana llahi mara mia moja (100), kisha ataandikiwa mema elfu (1000), au atafutiwa makosa elfu moja (1000)".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفوائد ذكر الله عز وجل
"Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفضائل أعمال القلوب، الأخلاق الحميدة، الزهد والورعموضوعات الحديثالزهد وقِصَر الأمل، الإخلاص، التقوى
"Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالأدعية المأثورة
"Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
التصنيف الشرعيفضائل أعمال القلوب، الأربعون النووية، تزكية النفوس
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالأدعية المأثورة
"Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالأدعية المأثورة