Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 110 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu huyu muuaji anaeleweka, na vipi kuhusu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Atakayesema: (Laa ilaaha illa llahu, wah-dahu laa sharika lahu, Lahul mulku, Walahul hamdu, Wahuwa alaa kulli shaini Qadiir) kwa siku mara mia moja, inakuwa kwakwe ni sawa na kuacha huru watu kumi, na anaandikiwa mema mia moja, na anafutiwa makosa mia moja, na inakuwa kwake ni kinga kutokana na Shetani kwa siku yake nzima mpaka afike jioni, na hatokuja yeyote na jambo bora zaidi kuliko atakalokuja nalo, isipokuwa yeyote atakayefanya zaidi ya alivyofanya yeye".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake