Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 50 kati ya 839

Ondoa vichujio
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Alikaa itikafu Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akawasikia wakidhihirisha kisomo, akafunua pazia, akasema: "Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi, na wasinyanyue sauti baadhi yenu kwa wenzao katika kisomo", au alisema: "Katika swala".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud
"Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
“Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake