Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 32 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!", Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi, akasema: hakuweza tena kuunyanyua kwenda kinywani kwake.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake