Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 2 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Nilikuwa nikihudumia watu vinywaji katika nyumba ya Abuu Twalha, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, akaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kunadi akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Abuu Twalha akasema kuniambia: Toka, nenda kaimwage, nikatoka nikaimwaga, ikatiririka pombe mitaro ya Madina, baadhi ya watu wakasema: Wameuliwa baadhi ya watu na pombe ikiwa tumboni mwao, Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na akafanya matendo mema katika vile walivyokula" [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilikuwa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mtu mmoja akasema, si jali ni amali gani nitakayoifanya baada ya Uislamu isipokuwa nitawapa maji mahujaji, na mwingine akasema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya Uislamu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na mwingine akasema: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yote mliyosema, Omari akawakemea, na akasema: Msinyanyue sauti zenu mbele ya Mimbari ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na hali yakuwa pia ni Ijumaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza kuhusu haya mliyotofautiana kwayo, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mnayafanya, enyi watu, yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuimarisha msikiti Mtukufu ni kama Imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho? [Tauba: 19] Mpaka mwisho wa Aya.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim