Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 27 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakika wewe unafunga milele, na unasimama usiku?", Nikasema: Ndiyo, akasema: "Hakika wewe ukifanya hivyo macho yatadhoofu, na nafsi itanyongeka, Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima", Nikasema: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hapo, akasema: "Basi funga swaumu Daudi amani iwe juu yake, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na wala hakimbii anapokutana (na adui)".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim