Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 14 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Imesimuliwa katika

Hakika mama Habiba bint Jahshi aliyekuwa chini ya Abdulrahman bin Auf alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu damu, akasema kumwambia: "Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga". Akawa akioga kila wakati wa swala.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالحيض والنفاس والاستحاضةموضوعات الحديثأحكام الغسل، أحكام الحيض والنفاس، أحكام الاستحاضة
Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيسنن الفطرة والسواك
"Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيفضل الوضوءموضوعات الحديثأحكام الوضوء
Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali.
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيأركان الوضوء، صفة الوضوءموضوعات الحديثأحكام الوضوء
Washirikina walisema kutuambia: Hakika mimi ninamuona jamaa yenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni kukidhi haja, akasema: Ndiyo, hakika yeye ametukataza kustanji mmoja wetu kwa mkono wake wa kulia, au kuelekea kibla, na akakataza kinyesi cha wanyama na mifupa, na akasema: "Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيالاستنجاء وقضاء الحاجة
“Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.” Akasema, nikasema: Ni kheri iliyoje hii, mara ghafla nikasikia msemaji mmoja mbele yangu akisema: Ile ya kabla yake ndio ilikuwa bora, basi nikatazama, mara nikamuona ni Omari, akasema: Nimekuona umekuja hivi karibuni, akasema: “Hakuna yeyote kati yenu atakayetawadha vizuri - au akaukamilisha vizuri- kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Pepo, aingie mlango wowote autakao".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
التصنيف الشرعيسنن وآداب الوضوء