Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 56 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe" Na katika sahihi Bukhari: Akasema: "Tawadha na uoshe tupu yako".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad