Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 55 kati ya 839

Ondoa vichujio
Washirikina walisema kutuambia: Hakika mimi ninamuona jamaa yenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni kukidhi haja, akasema: Ndiyo, hakika yeye ametukataza kustanji mmoja wetu kwa mkono wake wa kulia, au kuelekea kibla, na akakataza kinyesi cha wanyama na mifupa, na akasema: "Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
"Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba".
Sahihi Imepokelewa na Addar- Alqutni
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Punguzeni sharubu na mfuge ndevu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilimshuhudia Amri Bin Abii Hasan akimuuliza Abdallah Bin Zaidi, kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamimina katika mikono yake kutoka katika bakuli, akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akaingiza mkono wake ndani ya bakuli, akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga, kwa michoto mitatu, kisha akaingiza mkono wake akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake mara mbili mpaka katika viwiko viwili, kisha akaingiza mkono wake akafuta kichwa chake, akaanza upande wa mbele na akapeleka mpaka nyuma ya kichwa, mara moja, kisha akaosha miguu yake mpaka katika kongo mbili.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Aliniagiza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika haja fulani, nikapatwa na janaba, nikawa sikupata maji, nikajigaragaza katika udongo kama anavyojigaragaza mnyama, kisha nikamuendea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Nikamsimulia hilo, akasema: "Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hivi" Kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha ukapaka mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake