Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 8 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

"Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina, kwa sababu hali ya hewa ya Madina haikuwafaa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia wa zaka na wanywe mikojo yake na maziwa yake. Wakaondoka, na baada ya afya yao kurejea, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakaiba ngamia hao. Habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake mapema asubuhi, basi akatuma watu kuwafuatilia, na wakapatikana kabla ya mchana. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamuru mikono na miguu yao ikatwe, macho yao yakachomwa moto, na wakatupwa kwenye jangwa la mawe (Al-Harra). Wakawa wakiomba maji, lakini hawakupewa. Abu Qilaba anasema: Watu hawa walifanya wizi, wakafanya mauaji, walitoka katika Uislamu baada ya kuwa Waislamu, na walitangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Ya kwamba Jibril alimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Muhammad umetekesa kwa maumivu? Akasema: "Ndiyo" Akasema: "Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
"Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake