Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 32 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Asiache mapambo na kupendeza mwanamke yeyote kwa maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa mume wake atakaa miezi minne na siku kumi, na wala asivae nguo yenye urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, wala asipake wanja, wala asiguse manukato, isipokuwa atakapotwaharika anaweza kuchukua kiasi kidogo cha Qustwi au Adhfar (aina ya marashi ya kufukiza, hutumiwa na wanawake)".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.
Sahihi Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah kwa maana yake na Ahmad
"Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu, basi anaridhia kwenu: Mumuabudu yeye, na wala msimshirikishe na chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane, na anachukia kwenu mambo matatu: Umbeya, na kuuliza uliza sana, na kupoteza mali".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake