Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 10 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?" Wakasema: Tueleze, akasema: "Kusuluhisha kati ya watu, kwani kuharibika kwa mahusiano baina ya watu hilo hunyoa".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy
"Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akasema: "Ni umlishe pale unapokula, na umvishe unapovaa, au utakapopata kipato, na wala usipige uso, na wala usitoe maneno machafu, na wala usihame isipokuwa ndani ya nyumba".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
"Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake Hariri kwa mkono wake wa kushoto, na dhahabu kwa mkono wake wa kulia, kisha akazinyanyua kwa mikono yake, akasema: "Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao".
Sahihi Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn Majah
"Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
"Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad