Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 17 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili"
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Atakayejikatia haki ya muislamu kwa mkono wake wa kulia, basi Mwenyezi Mungu atakuwa kamuwajibishia moto, na kamharamishia pepo" Bwana mmoja akamuuliza: Hata kikiwa kitu kidogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kikiwa kijiti cha mswaki wa Araki".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia". Akasema: Akasema Al-Ash'athi: Kwangu mimi Wallahi kulitokea tukio hilo; kulikuwa na Ardhi baina yangu na bwana mmoja Yahudi, akanipinga kuwa si yangu, nikampeleka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuniambia: "Je una ushahidi?" Nikasema: Hapana: Akasema kumwambia Yahudi: "Toa kiapo". Anasema: Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sasa si ataapa na atachukua mali yangu!. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo..." mpaka mwisho wa aya.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake